Na Mwandishi wetu.
Wazee wa mapigo na mwendo kutoka mkoani Kigoma Mashujaa FC, wamefanikiwa kunasa saini ya Kocha Salum Mayanga akitokea Mbeya City FC ya Championship baada ya kumfuta kazi aliyekuwa Kocha wao Abdallah Mohamed Barres.
Mayanga, ambaye amefanikiwa kuiongoza Mbeya City kutinga hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho la CRDB baada ya kuwaondoa Azam FC kwa mikwaju ya penati kwenye dimba la Azam Complex.
Pia ameiwezesha Mbeya City FC kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Championship akiwa na alama 49 nyuma ya Mtibwa Sugar na kuwafanya mabosi wa Mashujaa FC kumuamini ili aweze kurudisha makali yao baada ya kuwa na matokeo yasiyoridhisha kwenye ligi kuu NBC.
#NTTupdates