×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MBUNGE IGHONDO ALETA MAKOCHA KUTOKA SWEDEN

Na Mwandishi wetu.

MBUNGE wa jimbo la Singida Kaskazini Ramadhan Ighondo, ametoa mafunzo kwa makocha na walimu wa michezo wa baadhi ya shule za Mkoa wa Dodoma, kutoka kwa Walimu wa makocha aliyowatoa Nchini Sweden lengo likiwa ni kuiibua na kukuza vipaji kwa vijana wenye umri wa miaka 5-19.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Oktoba 31 jijini Dodoma, katika shule ya msingi na sekondari ya Fountain Gate. Ighondo amesema lengo lake haswa yale magoli yanayolipiwa milioni 5 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan yaanze kutokea Singida.

“Tanzania sisi ni nchi tajiri hata ukiingia katika sekta ya michezo utaona namna Mama yetu Dkt. Samia anavyo thamini vipaji na analipa kila gori sasa nataka kuwahakikishia kwamba fedha hizo zitakuja jimboni kwangu kwani nimejipanga kutomuangusha Rais wetu, Licha ya kuwepo Mkoa wa Singida kwa siku mbili leo pia wamekuja kutoa fursa kwa Mkoa wa Dodoma pamoja na shule hii kwaajili ya kuhakikisha tunaibua na kukuza vipaji vya vijana wa umri wa miaka 5 kwenda juu mpaka miaka 19,”amesema.

Kwa upande wake Joseph Mjingo mwalimu wa Taaluma shule ya Fountain gate amemshukuru Mbunge wa jimbo la Singida kaskazini kwa kuona na kutambua thamani ya shule hiyo wanachokifanya.

“Ujio wa walimu wa makocha na walimu wa michezo katika shule yetu ni jambo nzuri na kubwa sana kwani sisi Fountain Gate naweza kusema ndio taasisi pekee Tanzania hii ambayo unaweza ukapata timu za aina zote kuanzia watoto wa miaka 3 na kuendelea lakini vile vile utapata timu za kuanzia miaka 5 na kuendelea,”amesema.

Naye Mwalimu Gaston kusenha ambaye ni mwalimu wa michezo kutoka shule ya msingi Brother Marthin iliyopo Dodoma akiwa ni miongoni mwa wanufaika wa mafunzo hayo amesema kuwa ushiriki wake katika mafunzo hayo utawasaidia walimu wa michezo kuwafundisha wanafunzi na waweze kupata uzoefu kuanzia wakiwa wadogo huku akitamani programu hiyo iende na katika maeneo ambayo bado haijafika.

#NTTupdates