×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MCHENGERWA AAHIDI UJENZI KITUO CHA AFYA MUNDARARA

Na Mwandishi wetu.

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa, ameahidi Serikali kutoa Shillingi million 300, Kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya kata ya Mundarara Wilaya ya Longido, Mkoa wa Arusha.

Mchengerwa ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na wananchi wa Mundara, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Mundarara Septemba 18, 2024 kufuatia ombi la wananchi hao kutokana na uhitaji mkubwa wa huduma ya Kituo cha afya katika eneo hilo.

Amesema kuwa lengo la Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kufikisha huduma muhimu zote kwa wananchi ikiwemo huduma za afya, elimu, miundombinu ya umeme, barabara na maji huku akisisitiza Serikali itatoa fedha na ujenzi utaanza mara moja.

#NTTupdates