×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MDEE- “MIAKA MITATU DAR ES SALAAM HAIJAPELEKA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO”

Na Mwandishi wetu.

IMEBAINISHWA kuwa katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo yaani kuanzia 2021-2023 Halmashauri 55 hazikutenga jumla ya Shilingi bilioni 38.8 kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) wakati akiwasilisha taarifa ya kamati kuhusu ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali, kwa hesabu zilizokaguliwa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 2023.

Mdee amezitolea mfano Halmashauri hizo ambazo ni sugu kuwa ni pamoja na Dar es Salaam ambayo kwa miaka hiyo mitatu mfululizo haijapeleka bilioni 21.7,Singida ni bilioni 2.3 Kigamboni walitakiwa kupeleka Bilioni 15.

Aidha Mdee amesema kuwa kamati hiyo imewataka wakurugenzi wote kuhakikisha fedha za miradi ya maendeleo zinapelekwa Kwa wakati.

#NTTupdates