×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MGOGORO WA KANISA NA SERIKALI WA ZAIDI YA MIAKA 30 WAFIKIA TAMATI

Na Mwandishi wetu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza kurejeshwa kwa eneo la mali ya kanisa katoliki Jimbo kuu Arusha Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu Jijini Arusha.

Akimuwalisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda leo Oktoba 17, 2024.

Amesema hatua hiyo imefikiwa mara baada ya kufikia suluhisho la mgogoro uliodumu kwa miaka 30 kati ya kanisa hilo na Serikali ulimfikia Mhe. Rais DKt. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mohamed Mchengerwa ambapo Serikali ilichukuwa eneo hilo kwaajili ya matumizi yake binafsi na kisha baadae kulitaka kanisa hilo kutoa Million 500 za kulipia eneo hilo kwa wakati kanisa hilo lilipoanza mpango wake wa kuongeza eneo kwaajili ya utoaji wa huduma mbalimbali kanisani hapo.

Naye Askofu Dkt. Issac Amani ambaye ni Askofu wa Jimbo kuu la Arusha ametoa shukrani zake za dhati kwa Rais DKt. Samia Suluhu Hassan kwa utatuzi wa changamoto mbalimbali za wananchi.

#NTTupdates