×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

“MGONJWA UNA HAKI YA KUJUA UNACHUNGUZWA NA KUTIBIWA NINI” -PROF.MAKUBI

Na Mwandishi wetu.

WAGONJWA wametakiwa kumuuliza daktari anachunguzwa na anatibiwa nini kwa sababu ni haki ya mgonjwa kujua tatizo linalomsumbua wakati anapoanza matibabu.

Akiongea na wagonjwa Siku ya Usalama wa Wagonjwa Duniani leo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Prof Abel Makubi, amesema anapaswa kuanza kujitambulisha kwa daktari halafu kueleza historia ya tatizo lake.

“Katika misingi yetu, madaktari tunaanza kumsikiliza mgonjwa.Unapoingia chumba cha daktari, mueleze daktari dalili zote na jinsi unavyojisikia kwa usahihi,” amesema

Mkurugenzi Mtendaji wa BMH.Prof Makubi amebainisha kuwa daktari atauliza maswali yake kwa usahihi kabla ya kukupima na kukuelekeza kufanya vipimo vya maabara au radiolojia.

“Wagonjwa wengi wanakimbilia kwenye vipimo, lakini mgonjwa anapaswa kuanza kumueleza daktari tatizo linalomsumbua,” amefafanua Prof Makubi.

Ndugu Salumu Bakari, mkazi wa Dodoma mjini, amepongeza huduma za BMH, akiongeza kuwa Bi Mwajuma Ramadhani amesema amekuwa akija kwenye Idara ya Mazoezi ya BMH, akipongeza kuwa hakuna sehemu anayocheleweshwa kwenye mchakato wa huduma BMH.

“Nakuja kila wiki kwa ajili ya mazoezi hakuna sehemu nimepata changamoto katika mchakato wa matibabu,” amesema Bi Mwajuma.

#NTTupdates