
Zaidi ya miche ya miti elfu tano imepandwa katika halmashauri ya jiji la mwanza huku wananchi wa jiji hilo wakisisitizwa kuilinda na kuitunza ili kukabilianana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi .
Akizungumza wakati wa kugawa miche hiyo ya miti kwa wananchi pamoja na kuipanda ikiwa ni sehemu ya kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya miti duniani mkuu wa wilaya ya nyamagana Amina Makilagi amesema miti hiyo inayopandwa na kugaiwa kwa wananchi ni kwa manufaa ya watoto na wajukuu kwa baadae ili waweze kunufaikanayo .

Nae Afisa Uhifadhi Misitu Wilaya ya Nyamagana Sharifa Kayonza amesema maadhihayo yameadhimishwa kwa kupanda miti elfu tano na kugaiwa kwa wananchi ambapo kila kaya imepatiwa miche mitano kwa ajili ya kupanda .
” lengo la kupanda miti hii na wanafunzi ni ili mwanafunzi akuwe na akili ya kutunza mazingira na kuhifadhi mazingira “
Kwa upande wake Devid Joseph Mkuu wa idara ya mazingira na maliasi halmashauri ya jiji la mwanza ameeleza lengo kuu la serikali na dunia nzima ni kuhakikisha mazingiara na uwasili wake unaifadhiwa na kutunzwa kwa ufasaha zaidi .
Khadija hamis na Ayubu Elias Wananchi wa kata ya isebanda wameeleza namna ambavyo wamefurahishwa na zoezi la ugawaji wa miche ya miti na kuahidi kuitunza miti hiyo ili kuweza kuboresha mazingira.
Kauli mbiu katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya miti duniani ni misitu ni uchumi kwa maendeleo ya taifa .










