×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MIKOA MINNE KUNUFAIKA NA MRADI MPYA WA EFFECTS PLUS

Na Mwandishi wetu.

Zaidi ya wakazi laki tatu wa Mikoa ya Mwanza ,Mara,Geita na Dodoma wanatarajiwa kunufaika na mradi mpya wa Effects plus unaolenga kuimarisha lishe na malezi kwa watoto pamoja na kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Mwanza na Meneja Mradi wa EFFECT PLUS Elfrida Kumalija wakati wa kikao cha kutambulisha mradi kwa wadau mbalimbali wakiwemo wataalam wa lishe,afya,ustawi na maendeleo ya Jamii ambapo amesema mradi huo ni wa miaka mitatu na utakwenda hadi mwaka 2028 Ukiwa na malengo ya Ushirikishwaji kwa wakina baba katika malezi ,lishe na kuondoa ukatili zaidi ya watoto.

Akizungumzia Mradi huo Mathias Shimo ambaye ni Meneja ufuatiliaji tathimini shirika la kutetea haki za wanawake na watoto Kivulini lenye makao yake makuu Jijini Mwanza amesema shirika hilo kwa kushirikiana na serikali amesema mradi huo unakwenda kutekelezwa katika ngazi ya jamii kwenye Halmashauri utakwenda kuhusisha Wanaume kwenye familia na kuleta tija kubwa.

Nae Mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza Dokta Jesca Leba amebainisha umuhimu wa mradi huo amesema bado wanachangamoto katika swala la lishe na wanaendelea kushirikiana na wadau katika kuboresha hali ya lishe kwa kushirikisha kina wanaume ambao ndio waamuzi wa mwisho katika familia.

Ushirikishwaji wa wanauwezo katika Mradi wa kuimarisha lishe na malezi kwa watoto pamoja na kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto ukawagusa wataalam wa maendeleo ya Jamii akiwemo Janeth Shishila afisa maendeleo ya Jamii mkoa wa Mwanza pamoja na Yusuph Omolo -afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Ilemela wamepongeza ujio wa mradi huo katika mkoa wa Mwanza kwani itaongeza uwelewa kwa Wanaume katika kujali familia zao.

Mradi huo wa EFFECT PLUS unaotekelezwa na shirika la kutetea haki za wanawake na watoto Kivulini lenye makao yake makuu Jijini hapa kwa kushirikiana na serikali watatekeleza mradi huo kwa Halmashauri 15 katika Mikoa yote minne ambapo itagharimu kiasi cha shilingi bilion 13 katika kipindi cha kuanzia Mwaka 2025 hadi 2028.

#NTTUpdates