×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MKOA WA MWANZA WAWEKA MIKAKATI KUKABILIANA NA UKATILI WA KIJINSIA

Na Mwandishi wetu.

Suala la maridhiano katika kesi za ukatili wa kijinsia Mkoani Mwanza limetajwa kufifisha juhudi za mapambano dhidi ya ukatili na kuchagia kesi hizo kuisha bila wahusika wa kutenda ukatili kuchukulia hatua.

Hayo yamebainihswa jijini Mwanza katika kilele cha maadhimisho ya siku kumi na sita za kupinga ukatili ambapo taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Wilbroad Mutafungwa licha ya kueleza matukio hayo kupungua lakini bado kuna changamoto ya maridhiano katika kesi hizo.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Amina Makilagi akizungumza katika maadhimisho hayo akabainisha mipango ya serikali katika kukabilina na kesi za ukatili.

#NTTUpdates