Na Mwandishi wetu.
Mkurugenzi wa kampuni maarufu ya utalii Gosheni Safaris, Peter Gosheni, amechukua rasmi fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge Katika Jimbo la Siha, Mkoani Kilimanjaro.
Peter Gosheni ni kielelezo hai cha mafanikio yanayojengwa kwa bidii, maarifa na maono thabiti, Kupitia kampuni yake ambacho imetoa mchango Katika kuitangaza Siha kitaifa na kimataifa, akileta fursa za ajira, kukuza utalii na kuhamasisha maendeleo endelevu.
Gosheni akiwa amekuja na kauli mbiu ya Siha Kwanza anaingia kwenye ulingo wa siasa akiwa na wito wa kweli wa kuleta mabadiliko chanya.
#NTTupdates