×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MNAPASWA KUWA MABALOZI WAZURI WA AMANI – RC MAKONGORO

Na Mwandishi wetu

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Charles Makongoro Nyerere, asisitiza wahitimu wa mafunzo ya awali ya kijeshi katika kambi ya mafunzo ya JKT Luwa iliyoko Mkoani Rukwa kuzingatia umuhimu wa kuwa mabalozi wazuri wa amani.

RC Makongoro ameeleza hayo wakati akiwa na wahitimu wa Operesheni Miaka 60 ya Muungano, Luwa.

Amesema wakati huu ambao wahitimu hao wa mafunzo katika kuimarisha ulinzi na usalama, wanahitimu huku Tanzania ikijiandaa kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Mkuu huyo wa Mkoa pamoja na viongozi wengine wa Serikali na vyombo vya ulinzi waliohudhuria hafla hiyo wamewapongeza wahitimu kwa kuwa na nidhamu katika kipindi chote cha mafunzo na kuwataka kuendeleza, kutunza na kuhifadhi mshikamano wa kitaifa uliopo.

#NTTUpdates