Na Mwandishi wetu.
Kuelekea kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la shirikisho Afrika (CAFCC) kati ya Mnyama Simba SC dhidi ya Stellenbosch FC ya Afrika Kusini kwenye uwanja wa New Amaan Complex Visiwani Zanzibar, Simba SC wamekuja na kauli mbiu mpya kwa ajili ya kuwapa hamasa ili kutinga fainali ya michuano hiyo.
“Kauli mbiu ya kuingia nusu ilikuwa HII TUNAVUKA na tukafanikiwa lakini kuelekea fainali tunakuja na HATUISHII HAPA.
Tunatoka hatua hii tunakwenda fainali. Malengo yetu ni kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.”-Meneja wa Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Ahmed Ally aliyasema hayo wakati anaongea na Waandishi wa habari kuelekea mchezo wao muhimu Visiwani Zanzibar.
#NTTUPDATES