Na Mwandishi wetu.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Alexander Mnyeti amewataka wafugaji na wananchi Kwa ujumla Wilayani Misungwi mkoani Mwanza kuhakikisha wanalinda mashamba ya uzalishaji ya Serikali na kutambua kuwa ni rasilimali muhimu kwaajili ya Maslahi mapana ya watanzania wote.
Naibu Waziri Mnyeti ameyasema hayo wakati wa ziara yake Katika shamba la uzalishaji Mifugo la Serikali mabuki lilipo Wilayani Misungwi huku akibainisha kuwa baadhi ya wafugaji sio waaminifu kwani makundi ya Ng’ombe Kutoka njee ya Wilaya hiyo yamekuwa yakiharibu mashamba ya Serikali.
Amesema wafugaji wanaoingiza Mifugo kwenye mashamba ya uzalishaji ya Serikali wanapaswa kuheshimu maeneo hayo kwa kuacha kufanya hivyo.
Kutokana na kitendo hicho Mnyeti amewataka wananchi ambao Wamekuwa wakishirikiana na wafugaji wanaovamia mashamba ya ufugaji Wilayani Misungwi kuacha tabia hiyo mara moja.
#NTTupdates