×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MO “HATUKUTENDEWA HAKI NA CAF ILA HATUJAKATA TAMAA”

Na Mwandishi wetu.

Rais wa heshima na Mwekezaji wa klabu ya Simba SC, Mohamed Dewji “MO” ametoa ya moyoni baada ya CAF kuwakatalia ombi la mchezo wa Fainali ya mkondo wa pili kati ya Mnyama Simba SC dhidi ya RS Berkane ya Morocco, kupigwa dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam na kupelekwa New Amaan Complex Visiwani Zanzibar.

Mwekezaji huyo, anaamini kuwa hawa kutendewa haki na wenye mamlaka za soka barani Afrika licha ya juhudi mbalimbali zilizofanywa na viongozi wa klabu, TFF na Serikali ili mchezo huo upigwe Benjamin Mkapa Dar es Salaam lakini ziligonga mwamba bila sababu za msingi.

Lakini pia Mwekezaji huyo ameendelea kuwatia moyo wachezaji wa klabu hiyo akiwataka waende New Amaan Complex Visiwani Zanzibar kuipambania nembo ya Simba SC ili waweze kubeba ubingwa na kuweka historia na heshima ya klabu hiyo.

#NTTupdates