Na Mwandishi wetu.
WANANCHI zaidi ya 300 wamepata huduma za matibabu ya kibingwa na ubingwa bobezi, kutoka kwa timu ya madaktari bingwa wa Rais Samia katika kambi iliyowekwa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda kwa siku nne.
Hayo yamebainishwa na Daktari wa kutoa dawa za usingizi na ganzi salama kutoka Hospitali ya Rufaa Landa ya Mbeya, Dkt. Letisia Komba ambaye pia ni sehemu ya timu hiyo ya Madakatari wa Rais Samia walioweka kambi ya siku saba katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi, Lengo la uwepo wa madaktari hao ni kuwahudumia wananchi na kutoa huduma za uchunguzi na matibabu kwa wananchi wa Manispaa hiyo.
“Tupo hapa hospitali ya Manispaa ya Mpanda ikiwa leo ni siku yetu ya nne tumeona mwitikio mkubwa wa wananchi kupatiwa huduma hizi za kibingwa na ubingwa bobezi,” ameeleza Dkt. Komba.
Amesema katika kipindi walichokaa wamehudumia wagonjwa wapatao 300 ambapo wametoa huduma za upasuaji kwa wagonjwa 11 wakiwemo wazazi na wenye magonjwa mengine na wananchi.
#NTTUpdates