
Kutokana na kukamilika kwa ujenzi wa Meli ya Mv New Mwanza wawekezaji katika sekta mbali mbali nchini ikiwemo sekta ya Utalii wameombwa kuitumia meli hiyo kuwekeza mkoani Mwanza kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla
Hayo yamesemwa na Msemaji mkuu wa Serikali Greyson Msigwa wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza juu ya miradi mbali mbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ya awamu 6 ikiwemo uboreshwaji wa huduma ya usafiri wa majini nan chi kavu
Msigwa pia ametoa wito kwa wawekezaji wa biasahara ya madini na Mazao mbali mbali kuhakikisha wanaitumia meli hiyo kukuza Uchumi wao
Aidha katika hatua nyingine Msigwa amesema kuwa serikali inaendelea kutoa fedha nyingi kwa mkoa wa Mwanza kwa ajili ya miradi mbali mbali ya maendeleo
Kutokana na mkoa huo kuwa wa kimkakati




