×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MSUVA AJIUNGA NA AL TALABA FC

Na Mwandishi wetu.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Simon Happygod Msuva (30) amejiunga rasmi na klabu na Al Talaba FC inayoshiriki ligi kuu Iraq.

Al Talaba imempatia mkataba wa mwaka mmoja utakaomuweka klabuni hapo mpaka 2025.

Msuva ambaye alikuwa akisakwa na vilabu kadhaa zikiwemo Simba SC na Yanga SC, lakini alitupilia mbali ofa hizo Kwani alikuwa na kiu bado ya kucheza nje ya Tanzania na Afrika kiujumla.

Vilabu ambavyo mpaka sasa Simon Happygod Msuva amevichezea kwenye ligi za ushindani ni 1. Azam FC (Tanzania) msimu wa 2010-2011

2. Moro United (Tanzania) mwaka 2011-2012.

3. Young Africans SC (Tanzania) mwaka 2012-2017.

4.Difaa El Jadida (Morocco) mwaka 2017-2020.

5. Wydad AC (Morocco) mwaka 2020-2021.

6. Al Qadsiah FC ( Saudi Arabia) mwaka 2022-2023.

7. JS kabylie FC(Algeria) mwaka 2023.

8. Al najma FC ( Saudi Arabia) mwaka 2023 na Sasa

9. Al Talaba FC (Iraq) klabu yake mpya na ataitumikia kwa msimu mmoja 2024 hadi 2025

#NTTupdates