×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MUTALE NJE WIKI MBILI

Na Mwandishi wetu.

KIUNGO mshambuliaji wa Simba SC, Joshua Mutale amepata majeraha yatakayomuweka nje kwa wiki mbili.

Kupitia Daktari wa Simba SC, Edwin Kagabo, amethibitisha kuwa kiungo mshambuliaji Joshua Mutale atakuwa nje kwa wiki mbili baada ya kupata maumivu ya nyama za paja katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Tabora United uliopigwa katika Uwanja wa KMC Agosti 18.

Dkt. Kagabo amesema”Mutale hajapata majeraha makubwa lakini ili kumlinda asiumie zaidi atakuwa nje ya uwanja kwa muda huo”.

#NTTupdates