Na Mwandishi wetu.
Mweyekiti wa Umoja wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha Ndg. Lempapa Lukumay ameendelea na ziara yake zakutembelea kata kwa kata katika Jimbo la Arumeru Magharibi ilikutatua kero za vijana.
Hii leo June 8, Lempapa Lukumay amefanya zira kata za Olmotonyi na Lengijave na kuwasikiliza Vijana wa kata hizo na kuwakata Vijana kuwa wavumilivu wakati kero zao zinatafutiwa majibu sahihi na kwa wakati.
Ikumbukwe Lempapa alitoa siku Kumi (10) za kutembelea kata zote huku akiwaasa Vijana kushiriki shughuli za kisiasa kwani hakuna maisha bila siasa kwani Vijana ndiyo nguvu Kazi ya taifa la kesho na kuhakikisha wanapambana na umaskini katika familia ,jamii na hata kitaifa.
Aidha amewahimiza vijana kushiriki katika miradi ya maendeleo katika kata zao ambayo imepelekwa katika kata zao kuitunza na kuilinda.
Kwa upande mwingine Lempapa amezungumzia mikopo Kwa Vijana huku akiwataka kuunda vikundi Kwa ajili ya kupata Mikopo ya Halmashauri.
#NTTupdates