Na Mwandishi wetu Dodoma.
SERIKALI imependekeza bajeti ya jumla ya shilingi trilioni 49.345.7 kwa mwaka 2024/25, ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 11.2 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2023/24 ya shilingi trilion 44.388.1.
Akiwasilisha katika kamati ya bunge zima mapendekezo ya mfumo na ukomo wa bajeti ya Serikali 2024/2025 leo Machi 11 bungeni jijini Dodoma Waziri wa Fedha Dkt.Mwigulu Nchemba amesema Kati ya mapato hayo, mapato yatakayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzaniayanakadiriwa kuwa shilingi trilioni 29.858.4,
Amesema Mapato yasiyo ya kodi yanayokusanywa na Wizara, Taasisi na Idara zinazojitegemea shilingi trilioni 3. 408.1 na mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa shilingi Trilioni 344.1.19.
“Mhe. Mwenyekiti makadirio ya mapato kwa mwaka 2024/25yamezingatia vigezo mbalimbali ikiwemo mwenendo halisi wa ukusanyaji wamapato mwenendo wa viashiria vya uchumi jumla na jitihada zinazoendeleakuchukuliwa na Serikali katika kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa mapato yandani.
“Amesema sehemu kubwa ya bajeti (asilimia 70.1) itagharamiwa na mapato ya ndani ambayo yanatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 10.0 mwaka 2024/25” amesema
Amesema Serikali itaendelea kuweka msukumo na jitihada za kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kuwa ndicho chanzo chenye uhakika na kisicho na masharti hasi katika kugharamia bajeti ya Serikali.
#NttUpdates