×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

NAMUNGO FC KURUDISHA MAKALI YAO LIGI KUU

Na Mwandishi wetu.

Klabu ya Namungo FC “The Southern Killers” imeahidi kurejea na nguvu mpya kwenye ligi kuu baada ya kuanza vibaya kwenye michezo miwili ya nyumbani.

Maneno hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mh. Hassan Ngoma amesema”Licha ya Namungo FC kupoteza michezo miwili ya ligi kuu dhidi ya Tabora United na Fountain Gate FC kwenye uwanja wa nyumbani lakini ameahidi watarejea na moto utawaka kwenye ligi kuu NBC 2024/2025″.

Ligi kuu NBC inaendelea ambapo leo Namungo FC, watacheza dhidi ya Dodoma Jiji FC kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati Mkoani Manyara.

#NTTupdates