×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

NAPOLI MABINGWA WA SERIE A 2024/2025

Na Mwandishi wetu.

Klabu ya SSC Napoli inayoshiriki ligi kuu ya Italy (Serie A) imefanikiwa kutangazwa mabingwa wa ligi hiyo baada ya kupata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Cagliari wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa armandro Maradona.

Licha ya kuwa na vita kali ya kuwania ubingwa dhidi ya Inter Milan, Napoli wamefanikiwa kubeba taji hilo wakifikisha alama 82, baada ya kucheza michezo 38, huku Intel Milan wakisalia nafasi ya pili wakiwa na alama 81 michezo ikiwa sawa na Napoli.

Napoli inabeba taji lake la 4 la serie A, chini ya Kocha Bora wa msimu huu Anthonio conte, huku tuzo ya MVP ikienda kwa kiungo wao MC Tominay kutokana na uwezo mkubwa alioonyesha kwenye klabu hiyo alipojiunga nayo akitokea Manchester United ya Uingereza.

#NTTupdates