Na Mwandishi wetu.
Nchi za Afrika ikiwemo Tanzania zimetakiwa kubuni mbinu bunifu, fikra chanya na mifumo thabiti ya kuwajengea uwezo Vijana kujitegemea Kwa kuwapa maarifa sahihi ya kukabiliana na Changamoto ya ukosefu wa ajira, mara baada ya kuhitimu vyuo vya elimu ya juu.
Kauli hiyo imetolewa jijini Mwanza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la umoja wa mataifa (UNDP) nchini Tanzania Shigeki Komatsubara wakati wa ziara yake katika chuo Cha Mipango ya Maendeleo vijijini.
Mwakalishi huyo amesema kuwa taifa lolote utegemea vijana kama nguvu kazi ya taifa hivyo wakiwa na uwezo wa kujitegemea na kujiajiri itasaidia kukuza uchumi na kuongeza ubunifu katika sekta mbalimbali hapa nchini.
Kwa upande wake mhadhiri wa chuo Cha Mipango ya Maendeleo vijijini Kituo Cha mafunzo Kanda ya Ziwa-Mwanza Daktari Bonax Mbasa amesema kuwa kwasasa wapo katika hatua za awali za kuanzisha Kituo maalumu Cha kutoa mafunzo ya ujasiliamali na ubinifu hili kuwasaidia vijana wanaomaliza vyuo kuwa na uwezo wa kujiajiri kote nchini huku mpango huo ukitarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni.
Nao baadhi ya wanafunzi wa Chuo hicho wamesema kuwa hatua hiyo itasaidia kukabiliana na changamoto za soko la ajira na Hali halisi ya Sasa.
#NTTupdates