Na Mwandishi wetu.
Winga wa klabu ya Santos na timu ya Taifa ya Brazil, Neymar Jr (33) amejiondoa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil kisa jeraha la goti na nafasi yake ulichukuliwa na nyota wa Real Madrid, Endrick.
“Kurudi kulionekana kuwa karibu sana lakini kwa bahati mbaya sitaweza kurudi kuvaa shati zito zaidi ulimwenguni katika wakati huu!”.
“Tulikuwa na mazungumzo marefu na kila mtu anajua hamu kubwa niliyonayo ya kurejea lakini tulifikia muafaka na kuamua kutojiweka hatarini ili nijiandae vizuri na nisiwe na majeraha kabisa!”
“Asante kwa wale walionitumia ujumbe wa msaada, ni sehemu ya mchakato”.Maneno hayo aliyasema Neymar Jr kupitia mtandao wa kijamii akielezea sababu ya kujiondoa kwenye timu ya Taifa na kuondoa sintofahamu kwa mashabiki wa Brazil.
Neymar atakosekana kwenye michezo miwili ya kuwania kufuzu kombe la Dunia 2026 ambapo Brazil atacheza na Argentina na Colombia.
#NTTupdates