Na Mwandishi wetu.
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimeahidi kuruhusu uraia pacha endapo kitapewa ridhaa ya kuongoza nchi, hatua ambayo wanasema inalenga kuwatambua watoto wanaozaliwa na wazazi wa mataifa mawili tofauti kuwa sehemu halali ya taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mgombea Urais wa chama hicho, Samandito Gombo, alisema suala la uraia pacha litakuwa miongoni mwa kipaumbele cha serikali ya CUF endapo itachaguliwa.
Aidha, Gombo alibainisha kuwa serikali yake pia itahakikisha watumishi wa umma hawataendelea kutaabika na mikopo ya ujenzi wa nyumba, badala yake serikali itasimamia ujenzi wa makazi yao ili kuwawezesha kuishi kwa heshima na utulivu.
#NTTUpdates