×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

NOELA LUHALA ATAMBULISHWA ASA TEL AVIV YA ISRAEL

Na Mwandishi wetu.

Beki wa timu ya Taifa ya Tanzania na klabu ya Young Princess, Noela Luhala (19), ametambulishwa rasmi kwenye klabu ya Asa Tel Aviv FC inayoshiriki ligi kuu ya wanawake nchini Israel.

Luhala, ambae alikuwa nahodha wa timu ya wasichana U-17 “Serengeti Girls” kwenye michuano ya kombe la Dunia la wanawake 2022 na kufanikiwa kucheza robo fainali ya michuano hiyo.

Idadi inaendelea kuongezeka kwa wasichana wanaocheza soka Tanzania kwenda kukipiga nje ya mipaka ya Afrika na wakiendelea kufanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali.

#NTTupdates