×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

NYOTA WA FILAMU ZA KIHINDI ASHAMBULIWA KWA KISU

Na Mwandishi wetu.

Muigizaji na Mtayarishaji wa filamu za kihindi (Bollywood) Saif Ali Khan (54) ameshambuliwa na mvamizi aliyekuwa na kisu nyumbani kwake katika eneo la Bandra jijini Mumbai.

Tukio hilo limetokea leo Alhamisi asubuhi mwendo wa saa 2:30 na mwigizaji huyo wa Bollywood alikimbizwa katika Hospitali ya Lilavati, ambako amefanyiwa upasuaji.

Taarifa ya polisi, inaelezea kuwa mvamizi huyo aliingia katika makazi ya mwigizaji huyo na kuanza kugombana na baadae kumshambulia kwa kisu.

#NTTupdates