Na Mwandishi wetu.
Timu ya Pamba jiji Fc ya jijini Mwanza hii leo July 30, 2025 imemtambulisha Fransis Baraza kua kocha mkuu wa timu hiyo akichukua nafasi ya Felix Minziro ambae alihudumu katika timu hiyo msimu uliopita.
Akimtambulisha kocha huyo mwenyekiti wa Timu hiyo Biko Kotecha amesema Kocha baraza amesaini mkataba wa mwaka mmoja na kama uongozi hawatamuingilia katika majukumu yake ya benchi la ufundi bali watatoa ushirikiano kwa kile atakachokua anakihitaji ndani ya timu hiyo.
Akizungumza mara baada ya kutambulishwa kocha Baraza amewaomba wachezaji mashabiki na viongozi wengine wa timu hiyo kumpa ushirikiano huku akisema malengo yake ni kuhakikisha timu ya Pamba inafanya vizuri na kushika nafasi za juu katika msimamo wa ligi kuu msimu ujao.
#NTTupdates