Na Mwandishi wetu.
Balozi na Mkuu wa Kituo cha Uwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Havana Cuba, pamoja na uwakilishi wa eneo la Karibe, Amerika ya Kati na nchi rafiki za Colombia, Venezuela na Guyana, Humphrey Polepole, amejiuzulu wadhifa huo Kwa kile alichodai kuwa hawezi kuwa sehemu ya uongozi usiohamasika na utii wa misingi ya katiba ya nchi, haki, maadili, utu na uwajibikaji Kwa Wananchi.
Kupitia barua yake amesema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya tafakari ya muda mrefu huku akiabainisha kuwa ataendelea kuwa mwanachama wa CCM wa kawaida na mzalendo wa kweli wa taifa lake.
“Uamuzi huu si mwepesi, bali umetokana na tafakari ya kina juu ya mwenendo wa uongozi katika nchi yetu, uzoefu wangu kama Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Novemba 2020-Machi 2022), na hatimaye kama Balozi,”amesema Polepole
Ameonheza kuwa kwa muda mrefu amekuwa akitafakari kauli ya CCM isemayo “Chama kwanza mtu baadaye”, mwanzoni mwa mwaka huu, nilipoona kauli hii inafanyika vinginevyo, nimejiuliza mara kadhaa ni maslahi ya nani yanapiganiwa wakati huu, mtu, kikundi au chama taasisi?
“Kwa kuwa siwezi kuendelea kuwa sehemu ya uongozi usiohamasika na utii wa misingi ya katiba ya nchi na chama, haki, maadili, utu na uwajibikaji kwa wananchi, nimeamua kwa hiari yangu kujiuzulu nafasi yangu ya uongozi na utendaji serikalini.”
“Nitaendelea kuwa mwana CCM wa kawaida, mzalendo na raia mwaminifu kwa Taifa na nchi yetu.” Ameongeza polepole katika barua yake.
#NTTupdates