×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

RAIS MSTAAFU AFRIKA KUSINI, ALIVYOTUA MOROGORO KWA SGR

Na Mwandishi wetu.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, mara baada ya kushiriki mhadhara katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, hii leo Mei 22, amewasili mkoani Morogoro kwa ziara maalum ya kutembelea eneo la kihistoria la Mazimbu, ambalo lilikuwa makazi ya wapigania uhuru wa Afrika Kusini waliokuwa uhamishoni wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi.

Mbeki amesafiri kwa kutumia Treni ya Kisasa ya SGR kuelekea Morogoro kwa ajili ya kutembelea eneo hilo lenye historia ya kipekee.

Akiwa Stesheni ya SGR ya Jakaya Kikwete, Morogoro, Mbeki amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

Ziara hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Afrika yanayoadhimishwa kila mwaka ifikapo Mei 25, kama kumbukumbu ya kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika (zamani ukijulikana kama OAU), pamoja na kuhamasisha mshikamano, maendeleo na utambulisho wa bara la Afrika.

#NTTUpdates