×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

RAIS MWINYI: MAZOEZI YANAONDOA MSONGO WA MAWAZO

Na Mwandishi wetu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, ameeleza kuwa Tafiti zimeonesha kuwa Mazoezi yanasaidia kwa kiasi kikubwa kujenga Afya ya Mwili ,afya ya akili na kuondoa Msongo wa Mawazo na kusisitiza jamii kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi kila siku.

Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza baada ya Kuongoza matembezi ya Afya yalioandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Taasisi ya Pharm Access ikiwa ni kampeni maalum ya kudhibiti Maradhi yasioambukiza kwa jamii yalioanzia Kiembe Samaki kwa Boutros hadi Uwanja Mao Tse Tung Wilaya ya Mjini.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuchukua juhudi maalum kuhakikisha inapunguza kasi ya ongezeko la Maradhi yasiombukiza hapa nchiniRais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa Takwimu za Wizara ya Afya zimeeleza kuwa kuna Ongezeko la Maradhi Yasioambukiza kwa kiwango kikubwa ikwemo Kisukari, Presha , Uzito na Unene uliopitiliza na shinikizo la damu kunakosababishwa na watu wengi kutofanya mazoezi.

Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa kutofanya Mazoezi kwa Wananchi walio wengi kunarejesha nyuma juhudi za Serikali za kudhibiti Maradhi hayo na kupunguza kasi ya kuleta Maendeleo.

Rais Dk.Mwinyi ametoa wito kwa kila mmoja kuchukua hatua ya kupunguza matumizi ya vyakula vya wanga na mafuta kukabiliana na maradhi hayo.

Kwa upande mwingine Waziri wa Afya Nassor Ahmed Mazroui amesema Dhamira ya Serikali ni kuona wananchi wote wana afya njema na kutambua kuwa suala la kufanya mazoezi sio anasa na Wizara inajiandaa kuwa na siku maalum ya mazoezi kila mwezi.

#NTTUpdates