×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

RAMOVIC ” PRESHA IMETUPA NGUVU YA KUJIANDAA VIZURI”

Na Mwandishi wetu.

Kuelekea mchezo wa kesho wa hatua ya makundi ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) utakaowakutanisha MC Alger ya Algeria dhidi ya Young Africans SC ya Tanzania nchini Algeria, Kocha wa Kikosi cha Wananchi ameahidi kufanya vizuri kwenye mchezo huo licha ya kuwa na presha baada ya kupoteza mchezo wa kwanza nyumbani dhidi ya Al Hilal Omdurman ya Sudan.

“Tuko kwenye presha baada ya kupoteza mchezo wa kwanza, lakini imetupa nguvu ya kujiandaa vizuri kuelekea mchezo wa kesho. Tumekuja mapema kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa.

“Hatuwezi kupanga matokeo ya mwisho yatakavyokuwa Lakini tunaweza kupanga jinsi tutakavyocheza ili kupata matokeo mazuri”.

“Yanga wana historia kwenye uwanja tutakaotumia kesho, walipoteza mchezo wa Fainali hapa kwa kanuni lakini naamini walishinda mioyo ya wapenda mpira hapa Algeria, kesho ni siku nyingine na tutakuja na nguvu nyingine ya kutaka kushinda mchezo”.

“Tunakwenda kucheza na timu ngumu, ina wachezaji bora na kocha mzoefu lakini upande wetu tuna kikosi chenye wachezaji bora sana, naamini itakuwa mechi nzuri yenye kuvutia.

“Maneno hayo yamesemwa na Kocha wa kikosi cha Young Africans SC, Sead Ramovic kwenye mkutano wa waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kesho.

#NTTupdates