×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

RAYO VALLECANO YAIDUWAZA REAL MADRID

Na Mwandishi wetu.

Rayo Vallecano imezima ndoto za Mabingwa watetezi wa Hispania (La Liga) Real Madrid ya kupanda kileleni mwa msimamo baada ya kufanikiwa kupata sare ya magoli 3-3 wakiwa nyumbani.

Magoli ya mchezo huo kwa upande wa Rayo Vallecano yamefungwa na U. Lopez dakika ya 4, A. Mumin dakika ya 36 na goli la mwisho likifungwa na I.

Palazon dakika ya 64 huku magoli ya Real Madrid yakifungwa na na Valvede dakika ya 39, Bellingham dakika ya 45 na Rodrigo dakika ya 56.

Sare hiyo imewafanya Real Madrid kusalia nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 17 akishinda michezo 11, sare 4 na vipigo viwili wakivuna alama 37 nyuma ya mahasimu wao FC Barcelona mwenye alama 38 kileleni mwa msimamo.

#NTTupdates