×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

RB LEIPZIG YATUMA OFA YA NOAH OKAFORI AC MILAN

Na Mwandishi wetu.

Klabu ya RB Leipzig inayoshiriki ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani imeanza mazungumzo na klabu ya AC Milan ya Italia ili kupata huduma ya mshambuliaji wa klabu hiyo Noah Arinzechukwu Okafori (24) raia wa Uswis.

Okafori ambaye anauwezo wa kucheza kama winga wa kushoto au mshambuliaji hajawa na msimu mzuri ndani ya AC Milan ambapo amecheza michezo 16, akifunga goli 1 na kutoa assist 2 kwenye michuano yote ambayo AC Milan imeshiriki.

Leipzig imepanga kumsajili mshambuliaji huyo ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chao ili kupambania ubingwa wa ligi hiyo msimu huu.

#NTTupdates