×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

RC BABU AZINDUA KLINIKI MAALUM YA SHERIA KILIMANJARO

Na Mwandishi wetu.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Kamati ya Ushauri wa Kisheria Mkoani Kilimanjaro Januari 21, 2025 wameandaa Kliniki maalumu ya Sheria bila malipo kwa wananchi wa mkoa huo.

Kliniki hiyo imezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nudrin Babu ambapo ameipongeza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kwa kuuchagua mkoa wa Kilimanjaro kuwa miongoni mwa mikoa inayopata huduma hiyo bure.

Aidha, RC Babu amesema kuwa ujio wa kliniki hiyo itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi kati ya wananchi wa mkoa huo pamoja na Serikali lakini pia kuwajengea uwezo wananchi wa kujua masuala ya kisheria.

Kliniki hiyo inatarajiwa kufanyika kwa siku saba kwanzia hii leo Januari 21 hadi 27, 2025 katika viwanja vya Stendi ya vumbi karibu na Stendi Kuu ya Mabasi ya Moshi.

#NTTupdates