×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

RC CHALAMILA AKABIDHI MILIONI 100 KWA AJILI YA UJENZI WA ZAHANATI YA SARANGA – UBUNGO

Na Mwandishi wetu.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo April 17,2025 amekabidhi milioni 100 kwa wakazi wa Saranga wilaya ya Ubungo ikiwa ni kutimiza ahadi aliyoitoa wakati amefanya ziara katika eneo hilo ambalo limekuwa likikabiliwa na changamoto ya Zahanati kwa kipindi kirefu licha ya kuwa na wakazi wengi wanaohitaji huduma ya Afya.

Vilevile RC Chalamila amekabidhi mifuko ya Saruji ili ujenzi wa zahanati hiyo uanze mara moja kwa kuwa tayari jengo hilo lilishaanza kujengwa kinachotakiwa kufanyika sasa ni ukamilishaji wa jengo hilo ili lifikie hatua ya kupaua.

Aidha kutokana na kitendo hicho wananchi wa eneo hilo wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jinsi anavyoboresha huduma ya mama na mtoto na kumuahidi mitano tena.

Katika nyakati nyingine mapema leo RC Chalamila ametembelea na kukagua barabara za Masaki wilaya ya Kinondoni ambapo amekemea vikali matumizi holela ya maeneo ya hifadhi ya barabara, uwekaji holela wa mabango ya matangazo barabarani, matumizi holela ya maeneo ya wazi, na ufanyaji holela wa biashara ambapo amesema Masaki ni eneo “Prime” kila kinachofanyika ni vema kuzingatia vigezo ambavyo ni rafiki.

Kwa upande Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Saad Mtambule amemhakishia Mkuu wa Mkoa kuyatekeleza maagizo yake mapema iwezekanavyo kwa masilahi mapana ya wakazi wa masaki Kinondoni, Mkoa na Taifa kwa Ujumla.

#NTTUpdates