Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenan Laban Kihongosi akiwa ameongozana na aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda, ambaye pia ni muasisi wa mashindano ya Samia Motocross Championship hii leo Julai 11, 2025 wametembelea viwanja vya Lakilaki Kisongo ambapo mashindano ya Samia Motocross Championship yanatarajiwa kufanyika hapo.
Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni ukaguzi wa maandalizi ya mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi rasmi kwanzia kesho Julai 12, 2025, katika viwanja vya Lakilaki, Kisongo Jijini Arusha.
#NTTupdates.