Na Mwandishi wetu.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuupa kipaumbele mkoa wa Arusha kwenye mambo mbalimbali ya Kitaifa kwani ni heshima kubwa kwa wananchi wa mkoa wa Arusha.
RC Makonda amesema hayo kwenye hafla ya mkesha wa Usiku wa Nyama Choma na Maadhimisho ya miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliyofanyika usiku wa Novemba 28, 2024 kuamkia leo Novemba 29, 2024 Jijini Arusha.
Aidha RC Makonda amemshukuru Rais Samia kwa kukubali mkoa wa Arusha kuwa kitovu cha Utalii huku akiahidi kuendelea kujadili namna bora ya kuleta maendeleo ya sekta ya utalii kwa majadiliano mbalimbali na wadau wa utalii ndani ya mkoa huo.
#NTTupdates