Na Mwandishi wetu.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda leo Novemba 27, 2024 ameungana na wakazi wa Mkoa huo kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwenye mtaa wa Mahakama Kata ya Sekei Jijini Arusha.
Mara baada ya kupiga kura, RC Makonda amewasisitiza wananchi wa mkoa wa Arusha kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi hili muhimu kwa kuchagua viongozi wanaofaa katika maeneo yao na wenye sifa za kuwa kiongozi.
Aidha, RC Makonda amewataka wananchi mara baada ya kumaliza kupiga kura waondoke vituoni na kuachana na jukumu la kulinda kura kwani jukumu hilo kisheria linabebwa na Mawakala wa vyama vya siasa vinavyoshiriki katika Uchaguzi.
#NTTupdates.