Na Mwandishi wetu.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda, amefanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo la Utawala la Halmashauri ya Jiji la Arusha na kuagiza mkandarasi anayesimamia ujenzi huo kuhakikisha anakamilisha kazi hiyo ifikapo mwezi wa tano mwaka huu tofauti na ilivyokuwa imepangwa hapo awali kukamilika mwezi Julai.
Makonda amesema hayo hii leo Januari 9, 2025 mara baada ya kupata taarifa Juu ya mradi huo kuwa umekuwa ukisuasua kukamilika bila ya sababu za msingi ili hali tayari kiasi cha Billion 6 za ujenzi huo zimeshatolewa.
Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Maximilian Iranghe pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa wamemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda, kwa namna ambavyo anakuza uwajibikaji kwa watumishi wa Mkoa huo huku wakiahidi kuendeleza ushirikiano uliyopo na wataalamu pamoja na watendaji wengine katika kusimamia maono na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ndani ya Mkoa wa Arusha.
#NTTupdates