Na Mwandishi wetu.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi nane (8) itakayopitiwa na Mwenge katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati.
Sendinga amefanya ziara hiyo hii leo, Julai 03, 2025 katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa kutembelea miradi hiyo nane akiwa ameambatana na Kamati ya maandalizi ya upokeaji wa Mwenge wa Uhuru mkoani humo.
Miradi hiyo iliyokaguliwa ni mradi wa kituo cha Afya Gallapo, mradi wa jokofu na kitanda cha kuoshea maiti, mradi wa daraja mamire, mradi wa ghala, mradi wa nishati safi na salama, mradi wa maji, mradi wa shule ya wavulana Manyara mradi wa usafirishaji pamoja na mradi wa kikundi cha Bajaji cha Magugu.
#NTTupdates.