×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

RC MTANDA AWATAKA WANANCHI KUTUMIA FURSA ELIMU YA WATU WAZIMA KUJIELIMISHA

Na Mwandishi wetu.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda, amewataka wananchi waliokosa elimu ndani ya mfumo rasmi kujielimisha kupitia fursa zitolewazo na mpango wa elimu ya watu wazima ili kupata uelewa.

Ametoa agizo hilo leo katika viwanja vya Mirongo Jijini Mwanza, wakati akihitimisha juma la elimu ya watu wazima, lililoadhimishwa kwa wataalam wa elimu kutembelea vituo vya kutolea elimu na ufundi stadi ndani ya Mkoa huo.

“Tungetamani kuona Wanamwanza na Watanzania wote waliokosa elimu kwenye mfumo rasmi wanapata elimu hiyo kupitia elimu ya watu wazima ili kuondoa ombwe la wananchi wenye elimu na waliokosa ili kuwa na usawa.” Mkuu wa Mkoa.

Amesema serikali inatambua umuhimu wa elimu nje ya mfumo rasmi kwa watu wazima kwa mchango wa ujenzi wa jamii zetu hivyo inawapongeza Wizara ya Elimu kwa usimamizi.”

Serikali inatambua mchango wa elimu ya watu wazima katika kupanua, kuimarisha na kuendesha huduma ya upatikanaji wa elimu kupitia fursa mbalimbali zilizopo”. Mkuu wa Mkoa

Naye Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndg. Kusirie Swai ametoa rai kwa magereza nyingine mkoani humo kuiga mfumo wa Magereza ya Butimba kwa kutoa elimu kwa wafungwa wanaoingia gerezani na kuwapatia ujuzi.

Juma hilo la wiki ya Elimu ya watu wazima limebeba kaulimbiu isemayo “Ujumuishaji wa Elimu Bila Kikomo kwa Ujuzi Ustahimilivu Amani na Maendeleo”.

#NTTupdates