ร—
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

REA YAWATAKA WANANCHI KUACHANA NA MATUMIZI YA KUNI NA MKAA

Na Mwandishi wetu.

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini REA Mhandisi Hassan Saidy amewaasa wananchi kuachana na dhana potofu ya kuwa nishati safi ya kupikia ni gharama kuliko nishati zingine kwani kwa Sasa teknolojia zilizoboreshwa ambazo zinazuia upotevu wa nishati wakati wa kupika.

Mhandisi Hassan ameyasema hayo katika maonyesho ya 49 ya biashara ya kimataifa(Sabasaba) jijini Dar-Es-Salaam wakati alipowatembelea banda la maonyesho ya wakala wa Nishati Vijijini (REA) huku akibainisha kuwa asilimia 96 ya Wananchi wa maeneo ya Vijijini wanatumia Kuni na mkaa kama nishati kupikia.

Kupitia taarifa yake amesema kuwa REA imewezesha jeshi la Magereza ambapo Magereza 129 zimehama kutoka kwenye matumizi ya Kuni na mkaa na wenda kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwa ni sehemu ya kutekeleza maagizo ya Serikali kuwa taasisi zinazohudumia watu zaidi ya 100 zianze kutumia nishati safi.

Kutoka na jambo hilo amebainisha kuwa mkakati wa taifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia umeelekeza ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati hiyo.

#NTTupdates