×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

REHEMA ABEBA TAJI LA PLOCK CUP 2024 POLAND

Na Mwandishi wetu.

Muwakilisha pekee wa mchezo wa tenesi kwa walemavu nchini Tanzania upande wa wanawake, Rehema Said ameendelea kupeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa baada ya kushinda kombe la Plock Cup 2024 nchini Poland akimshinda Agneska Tolocko kutoka Lithuania.

Rehema anaendelea kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali ya tennis anayoshiriki huku likiwa taji lake la pili mwaka huu baada ya kutwaa Kenya Open 2024, nchini Kenya Agosti 11, 2024.

Pia Rehema atashiriki michuano mingine ya Plock Open 2024 kuanzia leo Septemba 16 hadi 19 2024 nchini Poland.

#NTTupdates