×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

SENYAMULE ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI MIRADI YA AFYA NA ELIMU DODOMA

Na Mwandishi wetu.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ametembelea na kukagua miradi ya Elimu na Afya inayotekelezwa katika kata nne (4) ambazo ni kata ya Zuzu, Nala, Kikuyu kaskazini na Tambukareli zinazopatikana katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ziara hiyo, Senyamule ameutaka uongozi wa Jiji la Dodoma kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati hususani, miradi iliyotakiwa kukamilika katika kipindi cha mwaka wa fedha uliomalizika wa 2023/2024 na kuwataka kukamilisha miradi hiyo Ifikapo Mwishoni mwa mwaka huu na wananchi waanze kupatiwa huduma.

“Mnapopata fedha za miradi mnatakiwa mzitoe mapema ili kuikamilisha miradi kwa wakati kwasababu kumekuwa na uchelewaji wa kutekeleza miradi kunakotokana na mwaka wa fedha kumalizika, hivyo nitoe wito kwa Jiji kuhakikisha miradi yote inakamilika na inaanza kutoa huduma kwa wananchi kwa muda uliokusudiwa.

Awali akizungumza katika mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya Zuzu kinachotarajiwa kukamilika ifikapo Septemba 30, 2024 Senyamule ametoa maagizo kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanaanza mapema maandalizi ya kutumika kwa vituo vya afya kwa kufanya maandalizi yote Muhimu yanayohitajika.

#NTTupdates