×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

SERIKALI KUBORESHA TEHAMA SHULENI

Na Mwandishi wetu.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeandaa mpango maalumu utakaowezesha shule zote za Serikali kusimama imara katika matumizi sahihi ya TEHEMA ili kuwajengea uwezo wa maarifa ya kidigitali kwa wanafunzi wakiwa bado wako mashuleni.

Silaa amesema hayo leo Aprili 16, 2025 kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya TEHAMA kwa wasichana yaliyofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa ( AICC ) Jijini Arusha.

Kwa mwaka huu wa 2025 , Mafunzo hayo yamejumuisha jumla ya washiriki 248 kutoka katika kila mkoa wa Tanzania Bara na Visiwani huku yakifanyika kwa awamu mbili, awamu ya kwanza ikiwa ya kikanda katika kanda sita yaan Kanda ya Kati, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Pwani, Kanda ya Kaskazini pamoja na Kanda ya Visiwani Zanzibar huku awamu ya pili ikihitimishwa hii leo Jijini Arusha.

#NTTupdates.