Na Mwandishi.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Rashal Energies, Farhiya Warsame ambayo inajenga Bomba la Gesi kutoka Kisemvule hadi Mbagala jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matumizi ya vituo vya kujazia gesi kwenye magari (CNG) na viwanda.
Mazungumzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam tarehe Machi 6, 2025 kando ya Kongamano na Maonesho ya Petroli ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAPCE’25) linalofanyika kwa siku tatu jijini Dar es Salaam.
Dkt. Biteko amesema kuwa lengo la Serikali ni kuwa na mtandao mkubwa wa mabomba ya gesi pamoja na vituo vya kujazia gesi kwenye magari.
#NTTupdates