×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

SERIKALI: UCHUMI WA KWELI UNAJENGWA NA UWEKEZAJI WA WAZAWA

Na Mwandishi wetu.

Serikali imesema uchumi wa kweli wa nchi unapatikana pale wazawa wenyewe wanapowekeza kwenye nchi yao, ikiwemo ununuzi wa hisa kwenye kampuni mbalimbali kupitia Soko la Hisa la Mitaji la Dar es Salaam (DSE).

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, ameyasema hayo muda mfupi kabla ya kuzindua ushirikiano wa uuzaji hisa kwenye soko la DSE, ambapo kuanzia sasa mteja yeyote wa Benki ya NMB popote pale alipo duniani atakuwa na uwezo wa kununua hisa ya kampuni yoyote iliyosajiliwa kwenye soko la DSE, kupata taarifa, kujisajili, kufuatilia mwenendo wa soko na kuuza hisa zake kupitia App ya Benki ya NMB.

Kwa upande wao, Benki ya NMB kupitia Afisa Mtendaji Mkuu wake, Ruth Zaipuna, imesema moja ya ajenda ya benki hiyo ni kuhakikisha Watanzania wanashirikishwa katika kujenga uchumi wao binafsi na wa nchi kwa ujumla kupitia njia za kidijitali ambazo benki imewekeza.

Amesema kupitia App ya NMB, wanaamini wateja wao ambao kwa sasa ni zaidi ya milioni saba watakuwa na uwezo wa kushiriki ujenzi wa uchumi wa nchi yao kwa kununua hisa kwenye kampuni mbalimbali hapa nchini ambazo zimesajiliwa na DSE.

Benki ya NMB imesema itaendelea kuelimisha Watanzania ili wengi wao wawe na uelewa wa kutosha juu ya masuala ya kifedha na uwekezaji.

#NTTupdates