Na Mwandishi wetu.
Huduma ya mawasiliano inayoendelea kuimarishwa nchini,Serikali imeendelea kuridhishwa na kutoa wito kwa wananchi kuiitumia fursa hiyo kwa tija ya maendeleo.
Akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani Mwanza,Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Mhandisi Meryprisca Mahundi akizungumza na wakazi wa kijiji cha Sota kata ya Igalula Wilayani Sengerema sehemu uliojengwa mnara wa mawasiliano ameinisha huo ni miongoni mwa minara 758 ambayo Serikali imeweka nguvu yake kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya uhakika ya mawasiliano.
“Ndugu zangu huu ni mnara wa pili kujengwa hapa Wilayani Sengerema kwa ushirikiano wa Taasisi ya Serikali ya mfuko wa mawasiliano kwa wote USCAF na kampuni ya Vodacom,tuendelee kuiunga mkono Serikali kuhakikisha miondombinu hii inakuwa endelevu kwa maendeleo yetu na vizazi.
Aidha Mhandisi Mahundi amewataka wananchi kuacha kutumia mitandao ya kijamii kutapeli na kurusha picha sisizo na maadili kwani kwa watakao bainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yake Kwa upande wake Meneja Kanda ya ziwa kutoka USCAF Mhandisi Edward Benedict anabainisha miaka ya nyuma wananchi wa maeneo hayo walikuwa na changamoto ya kupata huduma ya mawasiliano, tofauti na sasa wana uhakika na shughuli zao za kiuchumi.
Awali kabla ya kuanza ziara wilayani Sengerema,Naibu Waziri huyo ametembelea Ofisi za kampuni ya TTCL zilizopo katikati ya Jiji la Mwanza Wilayani Nyamagana na kujionea kazi za mkongo wa Taifa na kutoa wito kwa wafanyakazi kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wateja wao na kuzitatua changamoto zinazojitokeza kwa haraka na siyo hadi atokee kiongozi na kupewa malalamiko.
Naibu Waziri huyo yupo katika ziara fupi mkoani Mwanza kukagua shughuli za mawasiliano zilizo chini ya Wizara yake baada ya kuhamishiwa akitokea Wizara ya Maji.
#NTTUpdates