×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

SERIKALI YATENGA BILIONI 4.83 KWA MRADI WA MABASI YAENDAYO HARAKA

Na Mwandishi wetu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mohammed Mchengerwa amesema Serikali imetenga Shilingi bilioni 4.83 kwaajii ya mabasi yaendayo haraka DART ambapo ambapo Shilingi bilioni 4.10 ni kwa ajili ya mishahara na Shilingi milioni 731.21 kwa matumizi mengineyo.

Mchengerwa ameyasema hayo leo Aprili 16,2025 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Amesema DART inapanga kukamilisha usanifu na ujenzi wa miundombinu ya awamu ya tano ya mradi wa mabasi hayo katika barabara za Nelson Mandela, Mbagala na Tabata-Segerea-Kigogo zenye urefu wa kilomita 26.

#NTTupdates